Lead

Sep 22 15 6:20 AM

Tags : :

 image
Mlanguzi mkuu wa madawa ya kulevya Brazil, Mario Sergio Machado Nunes 'O Goiano'  akiwa mikononi mwa wanausalama.
image
Mario Sergio Machado Nunes akiwa chini ya ulinzi.
image
wanausalama nchini Brazil baada ya kumtia nguvuni O Goiano.
WANAUSALAMA nchini Brazil wamemtia mbaroni mmoja wa walanguzi wakubwa wa madawa ya kulevya nchini humo.Mario Sergio Machado Nunes, ambaye pia anafahamika kama 'O Goiano' amekuwa mafichoni tangu atoroke jela miaka miwili iliyopita.
Polisi wanasema kuwa alifanyiwa upasuaji ili kubadili umbo lake na alikuwa akitumia stakabadhi bandia.Mnamo miaka ya themanini, O Goiano alikuwa kati ya watu wachache waliokuwa na uhusiano wa moja kwa moja na aliyekuwa mlanguzi maarufu wa madawa ya kulevya raia wa Colombia, Pablo Escobar.
Amekuwa akisafirisha madawa ya kulevya kati ya Marekani Kusini na Afrika.O Goiano alikamatwa akiwa katika jumba moja la kifahari katika mji wa pwani wa Guajura.Hapo jana, maafisa wa kupambana na mihadarati walitangaza kiinua mgongo cha dola milioni 5 kwa mtu yeyote atakayetoa habari zitakazopelekea kukamatwa kwa kiongozi wa genge la wauazaji mihadarati Joaquin Chapo Guzman ambaye kama Goiano alitoroka gerezani.